Tafadhali tuma nakala au kitabu (ngano, ushairi na wasifu, mkusanyiko wa hadithi fupiau, riwaya) iliyochapishwa katika miaka miwiki kabla mwaka wa tuzo kwa: kiswahiliprize@cornell.edu kabla ya Agosti, 5, 2019.
Mwandishi moja anaweza kutuma kazi moja pekee yake kila mwaka.
- Nakala hazifai kuwa chini ya maneno 50,000 kwa ngano na kurasa 60 kwa ushairi
- Kazi zote lazima ziwe katika Kiswahili
- Kazi zinafaa kutumwa kama faili ya Microsoft Word au Rich Text. Mada ya hadithi iwe jina la faili.
- Kurasa ya kwanza ya hadithi iwe na kichwa cha hadithi na hesabu ya maneno.
- Kazi ichapishwe kwa mtindo wa Times New Roman, ukubwa wa pointi 12 na nafasi kati ya mistari ya 1.5.
- Kazi zitumwe kama mwambatano wa barua pepe.
- Barua pepe inafaa kuwa na habari ifuatayo: Jina rasmi, Lakabu ya kuandika, Nambari ya simu, Tawasifu Fupi, Umri na Nchi ya Makazi
- Kwa kazi zilizochapishwa, tafadhali mwelekeze mchapishaji wako atume nakala tatu kwa Idara ya Masomo na Utafiti ya Afrikana (Africana Studies and Research Center, 310 Triphammer Road, Ithaca, NY 14850)