Tuzo ya Kiswahili ya Mabati Cornell ya Fasihi ya Kiafrika ilianzishwa na Mukoma Wa Ngugi na Lizzy Attree 2014 kuimarisha uandishi katika lugha za Kiafrika na kuhimiza utafsiri kutoka, kati ya na kwa lugha za Kiafrika. Tuzo hii inatoa mfano wa kihistoria wa ufadhili kwa Afrika kutoka Waafrika na kuonyesha kuwa hisani ya Kiafrika inaweza na inafaa kuwa kiini cha utungaji wa sanaa za kitamaduni za Kiafrika.”
Zaidi ya watu milioni 140 wanazungumza Kiswahili katika Afrika Mashariki na Kusini. Kiswahili pia ni mojawapo ya lugha rasmi Kenya na Tanzania. Kupitia waandishi na malenga mashuhuri wa Kiafrika wanaoandika katika Kiswahili kama vile Shaban Roberts na Ebrahim Hussein, kuna sanaa nyingi ya Kiswahili inayoendelea kutumika kama lugha kuu kwenye vyuo vikuu vya kusifika kama Chuo Kikuu cha Nairobi, Chuo Kikuu cha Boston na Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison. Yaani, Kiswahili ni lugha iliyosadikishwa na inafaa kutambuliwa hivyo.
Msimamo wetu ukiwa lugha zote ziliumbwa sawa na hakuna lugha inayofaa kufaulu kwa gharama ya lugha nyingine, tunapendekeza Tuzo ya Kiswahili ya Fasihi ianzishwe na lengo la kuimarisha kuandika na kusoma katika lugha za Kiafrika. Tuzo za fasihi zinatambua vipaji vipya, zinahimiza waandishi na kuonyesha kuwa kusoma ni muhimu.
Licha ya kuwepo tuzo za fasihi za kimataifa kama tuzo za Caine na Etisalat iliyoanzishwa majuzi, hakuna tuzo kuu za kimataifa na kiafrika zinazotuza sanaa zilozotungwa katika lugha za Kiafrika. Tuzo ya Fasihi ya Jomo Kenyatta ni tuzo ya mara mbili kila mwaka na inaandaliwa na Shirika la Wachapishaji wa Kenya (Kenya Publishers Association) kutambua kazi bora zilizochapishwa katika Kiingereza na Kiswahili.
Taarifa hio pekee yake inadokeza kwa nini tuzo ya kimataifa ya fasihi ya Kiswahili ni jambo la kihistoria na inatoa mfano kwa fasihi katika lugha zingine za Kiafrika na kuchangia pakubwa kwa fasihi duniani.
Tunawashukuru kwa usaidizi na subira yenu tunavyoendelea katika changamoto hii ya lugha.