Bodi ya Wadhamini

Mukoma-Jeremy Weate(1) photoMukoma Wa Ngugi, mwanzilishi mmoja, ni Profesa wa Kiingereza katika Chuo Kikuu cha Cornell na mwandishi wa Black Star Nairobi (Melville, 2013) na Nairobi Heat (Penguin, SA 2009, Melville House Publishing, 2011) na diwani ya mashari iitwayo Hurling Words at Consciousness (AWP, 2006). Yeye ni mwandishi wa This is Africa. Mukoma ana Shahada ya Udaktari katika Kiingereza kutoka Chuo Kikuu cha Wisconsin, Madison, Shahada ya Ufundi (MA) katika Uandishi wa Kubuni kutoka Chuo Kikuu cha Boston na Digrii ya Kiingereza na Sayansi ya Siasa kutoka Chuo cha Albright. Jarida la New African lilimtaja kama mmojawapo wa Waafrika 100 wenye wadhifa 2013.

Tafsiri ya Kijerumani ya Nairobi Heat ilitambuliwa na Buchkultur kama Kitabu cha Riwaya ya Uhalifu cha Msimu. Mwaka wa 2009, aliteuliwa mmojawapo wa washindi waliopendekezwa kushinda Caine Prize for African Writing Tuzo ya Caine ya Uandishi wa Kiafrika  na mwaka wa 2010 kwa Penguin Prize for African Writing kwa nakala ya riwaya yake, The First and Second Books of Transition. Riwaya mpya inayoitwa Mrs. Shaw itachapishwa karibuni na Ohio U/Swallow Press na Hunting Words with my Father (mashairi) kutoka Akiba ya Afrika ya Ushairi mwaka wa 2016. Tafsiri ya Kijerumani ya Black Star Nairobi itachapishwa karibuni.

Lizzy Attree photoLizzy Attree, mwanzilishi mwengine, ana Shahada ya Udaktari kutoka SOAS, Chuo Kikuu cha London, kwenye mada “Majawabu ya Kifasihi kwa UKIMWI kutoka Afrika Kusini na Zimbabwe kutoka 1990 hadi 2005”. Mahojiano yake na waandishi wa kwanza wa Kiafrika walioandika kuhusu UKIMWI kutoka Zimbabwe na Afrika Kusini yalichapishwa mwaka wa 2010 na Wachapishaji wa Wasomi wa Cambridge (Cambridge Scholars Publishing) na kuitwa ‘Blood on the Page’. Mwaka 2010, alikuwa Mhadhiri wa Kuzuru kwenye Idara ya Kiingereza kwenye Chuo Kikuu cha Rhodes iliyo Afrika Kusini. Kutoka mwaka 2002 mpaka 2009 alisimamia ziara za kifasihi za waandishi wa Kiafrika Uingereza zilizodhaminiwa na Baraza la Sanaa ya Uingereza (Arts Council England) kama vile Ziara ya Mwaka wa Kumi wa Tuzo ya Caine (Caine Prize 10th Anniversary Tour) mwaka 2009.

Aliteuliwa Msimamizi wa Tuzo ya Caine mwaka 2011 na kufanywa Mkurugenzi mwaka 2014. Atafundisha fasihi ya Kiafrika kwenye Chuo cha Kings London mwaka wa 2015 kama Mhadhiri wa Muda. Yeye ni mwanachama katika Baraza la Waakilishi la Writivism na ni mmojawapo wa waanzilishi wa Tuzo ya Kiswahili ya Fasihi ya Cornell-Mabati.

Abdilatif Abdalla Nov 12-13 photoAbdilatif Abdalla anajulikana zaidi kwa diwani yake ya mashairi ‘Sauti ya Dhiki’ (iliyochapishwa mwaka wa 1973) iliyoandikwa akiwa gerezani Kenya katika ya miaka 1969 na 1972. Alitiwa jela kwa kuandika kijitabu muhimu ‘Kenya: Twendapi?’ (1968) iliyoshutumu ukandamizaji wa serikali ya KANU ya Jomo Kenyatta. Abdalla pia amehusika na miradi mengi ya utafsiri na uhariri wa riwaya za baada ya ukoloni (Ayi Kwei Armah), tafsiri za Kurani, mashairi ya Kiswahili cha kale na kazi muhimu za kitaalimu huku akisimamia upinzani dhidi ya uongozi wa Moi alipokuwa uhamishoni London (na kina Ngugi) miongo ya 1980 na 1990.

WalterBgoya3Walter Bgoya, mwaka wa 1972 hadi 1990, Walter Bgoya alisimamia Nyumba ya Uchapishaji Tanzania (Tanzania Publishing House, TPH) iliyoimarisha Dar es Saleem kama eneo liloendelea kwa wasomi kimataifa. Mifano ya chapisho za TPH ni “How Europe Underdeveloped Africa” (Jinsi Ulaya Iliimaskinisha Afrika) ya Walter Rodney, “Sacred Hope” (Tumaini Tukufu) ya Agostinho Neto, “Establishing People’s Power to Serve the Masses” (Kuanzisha Nguvu za Umma Kuihudumia Jamii) ya Samora Machel na “Class Struggle in Tanzania” ( Vita vya Kitabaka Tanzania) ya Issa Shivji. Mwaka wa 1991, Bgoya alianzisha Mkuki na Nyota, kampuni huru ya kuchapisha vitabu ilioko Dar es Salaam. Bgoya alisema, kama jawabu kwa kutokuwa na uchapishaji huru wa kitaalimu Tanzania: “Tunajivunia kuchapisha vitabu muhimu, maridadi na vya bei rahisi na kuviweka kwenye mikono ya wasomi wenye hamu Tanzania na duniani.” Vitabu vya Mkuki na Nyota, vitabu vya watoto, vitabu vya biashara ya umma na vitabu vya elimu kwa Kiingereza na Kiswahili. Mchapishaji huyu anajitahidi kutafsiri fasihi kwa Kiswahili kwa mfano kitabu Kibwana Mdogo (The Little Prince) iliyo na asili ya Kifaransa. Bgoya ni mmoja wa waanzilishi wa Kikundi cha Vitabu vya Kiafrika (African Books Collective), kikundi kinachomilikiwa na kusimamiwa na wachapishaji wa Kiafrika. Mkuki na Nyota pia inashiriki na shirika zisizo za serikali (NGOs) kuimarisha kusoma na elimu Tanzania. Bgoya pia ni mwanzilishi wa Mtandao wa Wachapishaji wa Kiafrika (African Publishers Network) na alikuwa Mwenyekiti wa kamati ya kuamua ya Tuzo ya NOMA ya Uchapishaji Afrika (NOMA Award for Publishing in Africa). Walter Bgoya ametunga kazi nyingi za mada za kusoma, uandishi, uchapishaji na juhudi ya kutafuta sauti ya kweli ya Kiafrika katika dunia ya fasihi.

Happiness photoHappiness Bulugu ni mkufunzi wa Kiswahili Chuo Kikuu cha Cornell. Alipokea Udhamini wa Fulbright wa Kufundisha Lugha za Kigeni na Udhamini wa Shahada ya Pili katika Kufundisha kutoka Chuo Kikuu cha Oregon. Happiness ana Shahada ya Umahiri (M.A.) katika Utaalamu wa Kufundisha Lugha na Shahada ya Elimu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania. Ni mwanachama katika Shirika la Walimu wa Lugha za Kiafrika na Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU).

Anatoka Tanzania na hafundishi Kiswahili tu, bali anawajulisha wanafunzi wake kuhusu fasihi ya Kiswahili, na desturi na tamaduni za Kiswahili. Happiness pia anawafundisha na kuwatayarisha wanafunzi watakaosafiri Tanzania kupitia miradi ya Huduma Duniani (Global Service), Afya Duniani (Global Health) na Mradi wa Kiangazi Tanzania (Tanzania Summer Program) kuhusu itikadi na tamaduni za Kiswahili.

Chege Githiora photoChege Githiora ni Mhadhiri Mkuu wa Kiswahili katika Idara ya Lugha na Tamaduni za Kiafrika katika Chuo cha Masomo ya Maeneo ya Mashariki na Afrika (School of Oriental and African Studies), Chuo Kikuu cha London. Alizaliwa na kukulia Kenya na kusoma Meksiko na Marekani alikofundisha Kiswahili, lugha na fasihi, katika chuo cha El Colegio de Mexico, Chuo Kikuu cha Boston na Chuo Kikuu cha Michigan State alikohitimu na Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Kugha mwaka wa 1999. Anaandika na kutafsiri kutoka na kwa Kikikuyu, Kiingereza, Kiwahili na Kihispania. Mada za utafiti na machapisho yake ni uzungumzaji wa lugha zaidi ya moja, tofauti kati ya lugha, misimu ya barobaro mijini, Kihispania na tamaduni na jamii mseto za Kiafrika na Kihispania, hati na utafsiri. Juu ya hayo, anafundisha na kutafiti muundo wa lugha za Kibantu hasa Kikikuyu na Kiswahili.

Abdulrazak_GurnahAbdulrazak Gurnah alizaliwa Zanzibar, anahadhiri kwenye Chuo Kikuu cha Kent na anajulikana zaidi kama mwandishi wa riwaya. Riwaya yake ya nne Paradise (Peponi) ilikuwa mojawapo ya riwaya iliyopendekezwa kushinda Tuzo ya Booker mwaka wa 1994. Riwaya yake ya karibuni kabisa ni The Last Gift (Zawadi ya Mwisho). Mada yake kuu ya kielimu ni maandishi ya baada ya ukoloni na mada zinazohusiana na ukoloni hasa Afrika, Karibi na Uhindi. Amehariri kazi mbili za Essays on African Writing [Insha za Uandishi wa Kiafrika] (Heinemann) na A Companion to Salman Rushdie [Mwongozo wa Salman Rushdie] (Wachapishaji wa Chuo Kikuu cha Cambridge). Amechapisha nakala kuhusu waandishi wa kisasa baada ya ukoloni kama Soyinka, Naipaul na Rushdie. Alikuwa mwamuzi wa Tuzo ya Caine mwaka wa 2002 na mwenykiti wa waamuzi wa Tuzo ya Caine mwaka wa 2003.

Sarit Shah photoSarit Shah – Wasifu na picha itakuja karibuni

 

 

 

 

Ngugi Wa Thiong'o photoNgugi wa Thiong’o anafundisha kwenye Idara za Fasihi Linganishi na Kiingereza kwenye Chuo Kikuu cha California, Irvine. Alizaliwa Kenya katika familia kubwa ya wakulima wadogo na kusomeshwa Shule za Msingi za Kamandura, Manguu na Kinyogori kisha Shule ya Upili ya Alliance, zote zilizoko Kenya. Kisha Chuo Kikuu cha Makerere (iliyokuwa chini ya Chuo Kikuu cha London wakati huo), Kampala, Uganda; na Chuo Kikuu cha Leeds, Uingereza. Amepokea Shahada za Uzamivu saba za Heshima. Mtaalamu wa aina kadhaa, yeye ni mwandishi wa riwaya, insha, michezo na habari, mhariri, msomi na mtetezi wa kuboresha jamii. Ngugi ali­­­­pata kujulikana kwenye mandhari ya fasihi Afrika Mashariki kwa kuchezwa kwa mchezo wake mkuu wa kwanza, The Black Hermit (­­­­Mtawa Mweusi) kwenye Ukumbi wa Kitaifa wa Michezo Kampala. Aliandika Petals of Blood (­­­Vijani vya Damu), Decolonizing the Mind (Ukombozi wa Akili) na vitabu vingine. Ni mshindi wa Tuzo ya Fasihi ya Lotusna Tuzo ya Kimataifa ya Nonino ya Fasihi: aliteuliwa kwa Tuzo ya Kimataifa ya Man Booker.Mwaka wa 2012, alituzwa Tuzo ya National Book Critics Award kwa In the House of the Interpreter (Nyumbani kwa Mtafsiri) pamoja na Nicolás Guillén Lifetime Achievement Award for Philiosophical Literature. Mwaka wa 2010 and 2014, alikuwa ­­­mmojawapo wa waandishi waliopendekezwa kwa Tuzo ya Nobel kwa Fasihi.

Waakilishi zaidi watatangazwa

Skip to toolbar