Masharti ya Tuzo

Tuzo itatolewa kwa nakala bora ambayo haijachapishwa bado au kitabu kilichochapishwa katika miaka miwili kabla ya mwaka wa tuzo katika tanzu za ngano, ushairi na wasifu, na riwaya. Jumla ya $15,000 iliyopendekezwa kwa tuzo itagawanywa ifuatavyo:

Nafasi ya 1 katika ngano – $5,000

Nafasi ya 1 katika ushairi – $5,000

Nafasi ya 2 katika utanzu wowote – $2,500

Nafasi ya 3 katika utanzu wowote – $2,500

Kitabu au nakala itakayoshinda itachapishwa katika Kiswahili na Wachapishaji wa Kielimu wa Afrika Mashariki (East African Educational Publishers) na diwani ya mashairi bora itatafsiriwa na kuchapishwa kwa Kiingereza na Akiba ya Afrika ya Ushairi (Africa Poetry Book Fund).

Tamasha ya kutoa tuzo itafanyiwa Chuo Kikuu cha Cornell kwenye Idara ya Masomo na Utafiti ya Afrikana. Waandishi wanne watakaotuzwa wataketi Chuo Kikuu cha Cornell kwa muda wa wiki moja kisha wiki moja zaidi katika taasisi inayoshiriki (Marekani ama Afrika). Tamasha za pili na tatu zitafanyiwa Kenya na Tanzania mtawalia.

Skip to toolbar